Welcome to YTUnity

One free SpiderTaz Network account works across every network site.

RAIS SAMIA AWEKA MSINGI IMARA WA UKUAJI WA SEKTA YA BIMA NCHINI...

Global TV Online Video 2 days ago

Description

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imesema mageuzi yaliyotekelezwa katika sekta ya bima chini ya Serikali ya Awamu ya Sita yameongeza ufanisi wa taasisi hiyo na kukuza mchango wa sekta hiyo katika uchumi, huku ikizitaka kampuni za bima kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya mamlaka hiyo na maendeleo ya sekta ya bima nchini kwenye kikao kazi kilichoratibiwa na kuandaliwa na ofisi ya msajili wa hazina -OMH kati ya TIRA na wahariri wa vyombo vya habari Kamishna wa Bima Nchini, Dkt. Baghayo Saqware, amesema TIRA imeongeza gawio la Serikali kutoka shilingi bilioni 3.5 mwaka 2021 hadi shilingi bilioni 5.15 mwaka 2025, huku mapato yake yakiongezeka kutoka shilingi bilioni 11.18 hadi bilioni 21 katika kipindi hicho.
Akizungumzia utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, Dkt. Saqware amesisitiza umuhimu wa kampuni za bima kutumia nafasi zao na kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha mpango huo unawafikia wananchi wote, akieleza kuwa ushiriki wa sekta binafsi ni muhimu katika kupanua wigo wa huduma na kuimarisha kinga ya afya kwa Watanzania

============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com

Featured creators

Creators on the SpiderTaz Network

Become a creator →