Description
POLISI AKASIRIKA BASI KUZIDISHA ABIRIA: "MKANDA ANAUTOA WAPI?" - MADEREVA NA MAKONDAKTA WABANWA...
Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani limefanya operesheni na ukaguzi mkali mkoani Singida, ambapo askari wa usalama barabarani amembana dereva na kondakta wa basi baada ya kubaini wamepakia abiria waliokaa kwenye siti zisizo salama na zisizo na bima.
Katika ukaguzi huo, askari ameamuru abiria wote waliopakizwa kinyume cha sheria washushwe na watafutiwe usafiri mwingine salama, huku akiwakumbusha madereva kuhusu wajibu wa kulinda uhai wa abiria na umuhimu wa kufunga mikanda.
#UsalamaBarabarani #JeshiLaPolisi #GlobalTVOnline #Habari #TanzaniaTraffic #Singida
============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com
