Description
PAPA LEO XIV APIGWA ROZARI KARIBU NA JICHO WAKATI AKIWASALIMIA WAUMINI NCHINI PERU...
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, amepigwa usoni karibu na jicho na rozari iliyorushwa kutoka kwenye umati wakati akiwasalimia waumini mjini Lima, nchini Peru.
Tukio hilo limetokea katika siku ya mwisho ya ziara yake ya siku 12 katika bara la Amerika ya Kusini, ambapo maelfu ya waumini walikusanyika kumuona kabla ya misa ya kuaga. Licha ya kugongwa na rozari hiyo, kiongozi huyo hakusimamisha ratiba yake na aliendelea na shughuli za misa bila dalili za jeraha kubwa.
#PapaLeoXIV #KanisaKatoliki #HabariZaKimataifa #GlobalTVOnline #Peru
============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com
