Description
MAREKANI YALIPUA NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZA IRAN ZILIZORUSHWA KUELEKEA KAMBI YAKE YA BAHRAIN
Jeshi la Marekani kupitia Kamandi Kuu (CENTCOM) limethibitisha kufanikiwa kutungua na kuzuia mashambulizi ya ndege kadhaa zisizo na rubani (drones) zilizokuwa zimebeba vilipuzi, zilizorushwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) zikielekea nchini Bahrain.
Hatua hiyo inakuja huku Marekani ikikanusha madai ya Iran kwamba ndege hizo ziliharibu mifumo ya rada za kijeshi katika kambi ya anga ya Sheikh Isa nchini humo. CENTCOM imesisitiza kuwa hakuna uharibifu wa vifaa wala madhara yoyote kwa askari wake, huku vikosi vyake vikibaki katika hali ya tahadhari ya juu katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
#Marekani #Iran #Bahrain #CENTCOM #GlobalTVOnline #HabariZaKimataifa #SheikhIsaAirBase #Drones
============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com
