Description
MAREKANI YAISHAMBULIA IRAN - YALENGA KISIWA CHA QESHIM - BAADA YA SHAMBULIZI LA IRAN NCHINI BAHRAIN
Jeshi la Marekani limefanya mashambulizi ya kijeshi katika kisiwa cha Qeshm kilichopo kusini mwa Iran, ndani ya Mlango wa Bahari wa Hormuz. Mamlaka nchini Iran zimethibitisha kutokea kwa milipuko hiyo huku zikituhumu Washington kuhusika.
Picha na video zimeonyesha milipuko mikubwa na moshi ukipaa angani. Hata hivyo, Naibu Gavana wa Mkoa wa Hormozgan ameeleza kuwa operesheni hiyo haikuathiri maeneo ya makazi wala miundombinu ya kiuchumi. Fuatilia taarifa hii kwa undani kujua athari za kiusalama na kiuchumi katika eneo hilo muhimu la usafirishaji wa mafuta duniani.
#HabariZaKimataifa #Marekani #Iran #QeshmIsland #GlobalTVOnline #Marekani #Iran #Qeshm #GlobalTVOnline #HabariZaKimataifa #StraitOfHormuz
============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com
