Description
"KUNDI GUMU KULIKO YOTE" - HERSI ASEMA VIGOGO WALIVYOPANGWA NA YANGA CAF!
Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, amefunguka kwa kina kuhusu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) baada ya timu hiyo kupangwa kwenye kundi linalojumuisha vigogo watatu kutoka Kaskazini mwa Afrika: Zamalek (Misri), MC Alger (Algeria), na Club Africain (Tunisia).
Hersi ameweka wazi kwamba hili ndilo "kundi gumu kuliko yote", lakini akasisitiza kuwa Yanga ina kikosi imara na uwekezaji wa kutosha kupambana kufikia lengo kuu la kutinga hatua ya robo fainali. Pia amegusia safari ya mafanikio ya Yanga kufuzu hatua ya makundi mara nne mfululizo baada ya kusubiri kwa miaka 25.
#YangaSC #HersiSaid #CAFCL #LigiKuuBara #GlobalTVOnline #SokaTanzania #DaimaMbeleNyumaMwiko
============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com
