Description
KUFUTWA KWA TAASISI ZILIZOPITWA NA WAKATI: KIGOGO WA COSTECH ATOA KAULI NZITO!
Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 40 ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), uongozi wa taasisi hiyo umefunguka kuhusu mafanikio makubwa yaliyopatikana na mwelekeo wa nchi kuelekea Dira ya Maendeleo ya 2050.
Imeelezwa kuwa zaidi ya asilimia 70 ya malengo ya Dira ya 2050 yanategemea sekta binafsi, huku nafasi kubwa ikielekezwa kwa vijana wabunifu katika sekta za afya na kilimo. Pia, Waziri Mkuu anatarajiwa kuzindua ripoti ya kwanza ya mfumo mpya wa kukusanya na kuchakata taarifa za utafiti na ubunifu (NIST), pamoja na ujenzi wa miundombinu mipya ya kulea bunifu za vijana jijini Dodoma na Dar es Salaam.
#COSTECH #DiraYa2050 #UbunifuTanzania #WaziriMkuu #GlobalTVOnline #SayansiNaTeknolojia #TanzaniaNews
============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com
