Welcome to YTUnity

One free SpiderTaz Network account works across every network site.

#BREAKING: RAIS SAMIA AMTEUA DKT MPANGO KUCHUKUA NAFASI YA WARIOBA SUA - MABALOZI WAPYA WATAJWA!

Global TV Online Video Yesterday

Description

#BREAKING: RAIS SAMIA AMTEUA DKT MPANGO KUCHUKUA NAFASI YA WARIOBA SUA - BALOZI WAPYA WATAJWA!


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, ambapo amemteua aliyekuwa Makamu wa Rais Mstaafu, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA).

Dkt. Mpango anachukua nafasi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu, Mhe. Joseph Sinde Warioba ambaye amemaliza muda wake.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Ikulu, Rais Samia pia amemteua Bw. Ezekiel Mathias Goboro kuwa Kamishna wa Uhifadhi – Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), pamoja na kuteua Mabalozi wapya akiwemo Bw. Talha Mohamed Waziri, Bw. Lucas Aaron Mayanga, na Dkt. Miraji Ukoti Ussi.

#RaisSamia #DktMpango #UteuziIkulu #JajiWarioba #SUA #GlobalTVOnline #HabariMpya #BreakingNews






============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com

Featured creators

Creators on the SpiderTaz Network

Become a creator →