Description
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), akichukua nafasi ya Joseph Warioba aliyemaliza muda wake.
Uteuzi huo umetangazwa leo Jumanne, Novemba 17, 2026, kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu.
Katika uteuzi huo, Rais Samia pia amemteua Ezekiel Goboro kuwa Kamishna wa Uhakifadhi katika Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa).
Aidha, Talha Mohamed Waziri, ambaye ni mshauri wa Rais masuala ya demokrasia, ameteuliwa kuwa Balozi.
Wengine walioteuliwa kuwa mabalozi ni Lucas Mayanga na Dk Miraji Ussi, ambao watapangiwa vituo vya kazi.
