Description
RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA MAAFISA WAANDAMIZI WA POLISI IJUMAA HII MKOANI KILIMANJARO
Jeshi la Polisi nchini linatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Maofisa Waandamizi wa Polisi kuanzia Novemba 20 hadi 22, 2026, katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Lengo kuu la mkutano huu ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuweka mikakati thabiti ya kuimarisha ulinzi na usalama nchini kwa kushirikiana na wananchi.
#JeshiLaPolisi #RaisSamia #PolisiTanzania #UraSaccos #GlobalTVOnline
============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com
