Description
VURUGU ZAIBUKA NDANI YA NDEGE BAADA YA MWANAUME KUDAIWA KUTAKA KUITEKA - YABADILI NJIA KWA LAZIMA
Ndege ya shirika la American Airlines (Flight 1494) iliyokuwa ikisafiri kutoka San Diego kuelekea Chicago nchini Marekani, imelazimika kubadili njia na kutua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Phoenix Sky Harbor baada ya mwanaume mmoja kuzua taharuki na kudaiwa kutaka kuchezea mlango wa dharura ndani ya ndege hiyo.
Mashahidi na abiria walishirikiana na wahudumu wa ndege kumdhibiti abiria huyo kwa kumfunga mikono kwa kamba za plastiki na tepu hadi ndege ilipotua salama. Maafisa wa polisi na FBI wanaendelea na uchunguzi kubaini sababu za tukio hilo.
#GlobalTV
#HabariZaKimataifa
#AmericanAirlines
#TaharukiYaNdege
#HabariZaHiviPunde
============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com
