Aslay - Kapeperuka (Official Lyric Video)

Aslay Video 1 months ago

Description

https://Aslay.lnk.to/MyWay
https://www.facebook.com/AslayOfficial
https://www.instagram.com/aslayisihaka/
https://www.tiktok.com/@aslayisiaka

"KAPEPERUKA LYRICS

Nililifuma penzi kwa uzi wa chuma
japo sina kucha alipowashwa nilimkuna
Kuna muda aliumwa Hosptali ugonjwa hawakuona
Nikafata wagonga Moro Tanga na Kigoma akaponaaa
akapona yeye
Nilifubaa nilichakaa kusudi asije lala na njaa
na nilifanya mpaka kang’aa
walioncheka walimshangaa
Kapata mabawa karuka matawi kindege
Kabeba hadi ndala sasa chooni naendaje
eeeeh

Nilijua nitakula mwenyew chakula nilichopika
kumbe nilijenga barabara kila mtu anapita
Kasuku uko wapi wewe
Nilyekuita Malaika
mi nilijuaga masihara kumbe ndo unaniponyoka umekwenda

Kapeperuka
Kapeperuka
kaniachia maua
Kapeperuka
Kapeperuka
Kipepeo
Kapeperuka
Kapeperuka
Taabani naugua
Kapeperuka
Kapeperuka
hoi hoi oooh
yeyeye
lelelelele


angesema mapema nisingejisumbua
ningemwacha afe tu wakati anaugua
Nilipoteza muda wangu kumtibiaa
kwakujua atakuwa wangu eti kanikimbia
Nasikia anakula ananenepa
Mwenzake nalialia nimebaki mifupa
jama naugua naugua
Nilie mtegemea jamani kanitupa

Wanasema cha mtu mavi ukikiona kitemee mate
ila cha kwangu asali wakitafuna kwa mkate
Kapata mabawa karuka matawi kindege
Kabeba hadi ndala sasa chooni naendaje
eeeeh

Nilijua nitakula mwenyewe chakula nilichopika
kumbe nilijenga barabara kila mtu anapita
Kasuku uko wapi wewe
Nilyekuita Malaika
mi nilijuaga masihara kumbe ndo unaniponyoka umekwenda

Kapeperuka
kapeperukaaaa
kaniachia maua
kapeperuka
kaperukaa
kipepeo wangu jamaan
kipepeooo
Kapeperuka
kapeperuka
taaabani nauguaaa
kapeperuka
kapeperuka
hoi hoi oooh
aaaaaah aaaaah "